Swahili Videos

Wamiliki wote wa bunduki kujisajili upya kufikia Disemba 17

Mkenya yeyote anayemiliki bunduki kuanzia tarehe 17 Disemba anahitajika kusajiliwa upya ili kumiliki bunduki hiyo, huku ikiaminika bunduki elfu 30 zinamilikiwa kinyume cha sheria na wanasiasa na wafanyibiashara mashuhuri.
Kupitia waziri wa usalama wa ndani, ni kuwa zoezi hili linalenga kumaliza ongezeko la bunduki haramu nchini, hivyo basi kila mmoja anayemiliki bunduki atahitajika kukaguliwa, kusajiliwa na kupewa leseni upya kuanzia tarehe hiyo.
Siku tisini baada ya tarehe hiyo, atakayekuwa hajafanya hilo atajipata pabaya pa mkono wa sheria, kwani bunduki hiyo itakuwa haramu.

Show More

Related Articles