Swahili Videos

Genge la uhalifu lawaua watu 3 Kisauni Mombasa

Huku sikukuu ya Krismasi ikibisha hodi na idara ya polisi kuwahakikishia wakenya usalama wao,watu watatu wameuawa na genge la wahalifu mtaa wa Kisauni Mombasa.
Kulingana na polisi,ni kuwa watatu hao waliuawa na majambazi waliokuwa wamejihami kwa vifaa butu wakati wa jaribio la kuvamia na kupora duka mpoja la M-pesa.
Hayo yakijiri inspekta jenerali wa polisi amewaagiza maafisa wa polisi wa trafiki kuwapokonya leseni madereva walevi na wale watakaopatikana wakiendesha magari kiholela ili wachukuliwe hatua na NTSA.

Show More

Related Articles