Swahili Videos

Ajali ya ndege Ethiopia : Vipande vya miili vilivopatikana ni zaidi ya elfu 5

Chembe chembe za jamaa za wahanga wa ajali ya ndege ya Ethiopia zimekusanywa, ili zifanyiwe uchunguzi wa DNA.
Haya yamejiri huku ikibainika kwamba huenda ikachukua muda wa miezi 6 kupata matokeo ya uchunguzi huo.
Waokoaji kufikia sasa wamefanikiwa kupata vipande zaidi ya elfu 5 vya miili ya abiria 157 waliofariki kwenye ajali hiyo.
Hii leo wanahabari wamekuwa na kibarua kigumu kunakili taarifa zozote kuhusu mkasa huo baada ya serikali ya Ethiopia kupiga marufuku unakili wowote kwenye mkutano uliotibuka baina ya familia hizo na wasimamizi wa shirika la ndege la Ethiopia.

Show More

Related Articles