Maafisa 7 wa polisi kuchukuliwa hatua kuhusiana na ajali ya barabarani inayoshukiwa kumhusisha mhubiri James Nganga

Maafisa saba wa polisi wamependekezwa kupigwa kupigwa kalamu kwa  kujaribu kuficha ukweli kuhusiana na ajali ya barabarani, inayoshukiwa kumhusisha  mhubiri  James Nganga , huku  uchunguzi wa idara ya polisi vilevile ukipendekeza Nganga pia ashtakiwe .  Faili  ya kesi hiyo  itakabidhiwa mwendeshaji mkuu wa mashtaka Keriako Tobiko hapo kesho. Haya ni kwa mujibu wa inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet.  Nganga ameendelea  kusisitiza kuwa hana hatia  kuhusiana na  ajali hiyo , iliyopelekea kifo cha mwanamke mmoja, huku mumewe akijeruhiwa  vibaya.

Also read:   Mume amng’oa jicho mkewe kwa kudaiwa pesa,Bungoma

Related Articles