MakalaMilele FmSwahili

Wazazi washauriwa kupeleka wanao wa kike waliotimu miaka 9 kupata chanjo ya HPV

Iwapo mwanao wa kike ametimu miaka 9 na zaidi,basi unashauriwa wewe mzazi kumpeleka mwanao kupewa chanjo ya kuzuia virusi vya Human Papilloma (HPV) ambavyo husababisha saratani ya uzazi (Cervical Cancer).Hii ni kutokana na takwimu zinazoonyesha kwamba mtoto wa kike anaweza kupatwa na saratani ya uzazi miaka ya baadaye kutokana na virusi hivyo.

Takwimu za wizara ya afya  nchini zinaonyesha zaidi ya wanawake 3,000 hupoteza maisha kutokana na saratani ya uzazi(Cervical Cancer) kila mwaka.Ni kutokana na takwimu hizi,wizara ya afya inapanga kuzindua chanjo  ya virusi vya Human Papilloma virus(HPV) ambavyo husababisha aina hiyo ya saratani kwa asilimia 99.7.

Kulingana na wataalamu wa afya,virusi hivyo huwa mwilini kati ya miaka 15 hadi 20 na huathiri wanawake kuanzia miaka 9 hali ambayo sasa madaktari wanawataka wazazi kuwapeleka kupewa chanjo ya kuzuia kupatwa na saratani ya uzazi katika maisha yao ya baadaye.Daktari catherine nyongesa anasema saratani ya uzazi inaweza kutibiwa ikiwa utapatikana kwa mapema,ukiwa na tiba tofauti kulingana na makali yake.

Baadhi ya waathiriwa ambao nilizungumza nao wakinieleza matumaini yao na changamoto wamepitia sasa wakiwarai wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo.Aidha zipo njia zingine za kujikinga na saratani hii kama kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara,hapa Kenya asilimia 16 ya wanawake hukaguliwa mara kwa mara idadi ambayo ni ya chini sana huku wakiwalenga wanawake kati ya miaka 25 na 49.

Show More

Related Articles