HabariMilele FmSwahili

Watu 2 wakamatwa wakifyonza mafuta katika bomba la Kenya Pipeline, Machakos

Polisi wanawazuilia wanaume wawili waliofumaniwa wakifyonza  mafuta kutoka bomba la kampuni ya mafuta ya Kenya Pipeline katika eneo la Kathangaita, kaunti ya Machakos. Idara ya DCI aidha imedhibitisha kunasa lori moja ambalo washukiwa walitumia kusafirisha mafuta hayo wakidai kuwa ni maji. Akizungumza baada ya kuzuru eneo la tukio kaimu meneja mkurugenzi wa  Hudson Andambi amedhibitisha kuwa polisi wanamnasa mshukiwa mwengine aliyeponyoka mtego wa polisi.

Show More

Related Articles