HabariMilele FmSwahili

Watahiniwa 4 wa KCSE wapigwa marufuku kwa tuhuma za udanganyifu

Watahiniwa wanne wa mtihani wa kidato cha nne wamepigwa marufuku kukalia mtihani wa KCSE unaoendelea na majina yao kuondolewa kwenye sajili ya watahiniwa. Akizungumza mjinji Naivasha kaunti ya Nakuru ambapo ameshuhudia kufunguliwa kwa makasha ya mitihani hiyo, waziri wa elimu Balozi Amina Mohamed amesema watahinwa hao walikamatwa wiki jana baada ya kupatikana na simu za rununu ndani ya vituo vya mtihani. Waziri amewataka wasimamizi wa mtihani kuwakagua vilivyo watahiniwa wote ili kuzuia visa hivyo.

Katibu wake dkt Belio Kipsang akizungumza mjini Mombasa ameelezea kuridhishwa na mikakati iliyowekwa kudumisha uadlifu wakati wa mtihani huo.

naye mwenyekiti baraza la mtihani nchini KNEC profesa George Magoha amewaonya wasimamizi wa vituo vya mtihani dhidi ya kuhusika katika njama yoyote ya wizi wa mtihani

Show More

Related Articles