HabariMilele FmSwahili

Watahiniwa 2 wa kwanza katika mtihani wa KCPE mwaka huu wapata alamu 453

Wanafunzi 2 ndio waliofanya bora katika mtihani wa  KCPE mwaka huu kila mmoja akipata alama 453. Waziri wa elimu Balozi Amina Mohamed akitangaza ramsi matokeo ya mtihani huo uliofanywa mapema mwezi huu, anasema watahiniwa waliopata zaidi ya alama 400 mwaka huu pia  waliongezeka kutoka 9,846 mwaka jana hadi elfu 12,273 mwaka huu

Akizindua matokeo hayo, katika shule ya Star Of The Sea kaunti ya Mombasa, Amina anasema hakuna kisa cha udanganyifu kilivyoshuhudiwa katika mtihani huu japo matokeo ya watahiniwa 4 imefutiliwa mbali kwa kubainika walioshiriki mtihani huu sio watahiniwa halisi

Aidha Amina amepongeza kuimarika idadi ya watahiniwa wa kike mwaka huu ikilinganishwa na wenzao wa kiume.

Kadhalika Amina amelaani vikali wingi wa visa vya watahiniwa waliopachikwa mimba na kuwataka wazazi kuwajibika

Amina amedokeza zoezi la kuwapa nafasi katika shule za upili watahaniwa hawa litaanza desemba 3, akiwahakikishia wote waliokalia mtihani huu watapata nafasi katika shule za sekondari.

Show More

Related Articles