HabariMilele FmSwahili

Warsha ya mafunzo kwa walimu kufanikisha mtaala mpya wa elimu kuzinduliwa leo

Waziri wa elimu profesa George Magoha hii leo anatarajiwa kuzindua rasmi warsha ya mafunzo kwa walimu watakaofanikisha mataala mpya wa elimu wa 2-6-3-3. Warsha hiyo ya siku nne inatarajiwa kutoa mafunzo kwa zaidi ya walimu 90,000  walioteuliwa kutoka kote nchini. Warsha hii inakumbwa pingamizi kutoka kwa walimu chama cha KNUT kikiwaagiza walimu walio wanachama wake kutohudhuria.

Yakijiri hayo,waalimu sasa wanatisia kutoshiriki mafunzo muhula wa pili iwapo serikali itaendelea na azma yake ya kuwatoza asilimia 1.5 ya mishahara yao kufadhili ujenzi wa nyumba za bei nafuu.Katibu mkuu wa knut tawi la Tranzoia Dickson Okemwa anasema hii ni njama ya serikali kuwalaghai mshahara wao ambao ni finyu ilivyo kwa sasa.

Show More

Related Articles