HabariMilele FmSwahili

Wapiga mbizi kutoka Afrika Kusini wawasili Likoni kusaka miili iliyozama

shughuli ya kusaka miili ya mama na mwanawe waliozama katika bahari Hindi imerejelewa muda mfupi baada ya kusitishwa kwa muda ili kuzipa fursa meli za kijeshi kutoka India kutua nanga.

Mwenyekiti wa huduma za feri Dan Mwazo amesema shughuli hiyo kwa sasa inaendeshwa kwa mitambo ya kidijitali.

Aidha mwazo anasema wapiga mbizi kutoka Afrika Kusini waliokodishwa na familia ya Mariam Kighenda na mtoto Amanda Mutheu wamewasili. Wapiga mbizi hawa watashirikiana na kikosi cha wanamaji wa Kenya katika oparesheni ya kuwaska wawili hao ambao imeingia siku ya 9 leo.

Show More

Related Articles