HabariMilele FmSwahili

Wakenya milioni 31 wasajiliwa kwenye mfumo wa Huduma Namba kufikia sasa

Usajili wa wakenya kwenye mfumo wa Huduma Namba unakamilika Jumamosi hii. Waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiangi anasema uamuzi huo  unalenga kuokoa kitita kikubwa cha fedha ambacho hutumika kila siku kugharamia marupurupu ya maafisa wanaoendesha zoezi hilo.

Matiangi anasema iwapo mkenya atakosa kujisajili kupitia mfumo huu basi huenda akapoteza uwezo wa kupokea huduma muhimu za serikali.

Kufikia sasa Matiangi anasema wakenya milioni 31 wamejisajili kwenye mfumo huu wa huduma numba.

Aidha Matiangi anasema usajili wa wakenya walio nje ya nchi utakamilika Juni 20.

Show More

Related Articles