HabariMilele FmSwahili

Wafanyikazi katika kaunti 20 watarajiwa kuanza mgomo wao leo

Shughuli zinatarajiwa kutatizika hii leo katika  kaunti  20  iwapo wafanyikazi watagoma kulalamika kuchelewa mishahara yao ya mwezi  Julai. Katibu wa muungano wa wafanyakazi wa kaunti Roba Duba ameapa kutolegeza kamba hadi pale kaunti hizo zitakapowalipa wafanyakazi  kilicho chao. Duba akisema hamna kaunti iliyo na sababu ya kutofanya hivyo .

Mgomo huo utahusisha vyama nguli vya wafanyakazi kama kile cha wauguzi pamoja na bodi ya madaktari nchini KMPDB

Baadhi ya kaunti zinazotarajiwa kuathirika na mgomo huo ni pamoja na Nyeri, Muranga, Laikipia, Taita Taveta, Isiolo, Marsabit, West Pokot, Baringo,  Kericho, Elgeyo Markwet, Nakuru, Embu,Machakos, Tharaka Nithi, Bungoma pamoja na Kisumu.W

Show More

Related Articles