MichezoMilele FmSwahili

Tottenham yatangaza bei ya Victor Wanyama

Tukisonga mbele ni kwamba klabu ya Tottenham Hotspur imeweka bayana nia ya kumwachilia nyota wa Harambee Stars Victor Wanyama.

Ripoti kutoka London zinaarifu kwamba,Spurs iko tayari kumpiga bei wanyama kwa kima cha pauni milioni 17 na tayari Club Brugge ya Ubelgiji imeonyesha nia ya kumsajili.

Wanyama mwenye umri wa miaka 28 alisajiliwa na Tottenhma mwaka 2014 kutoka Southampton na angali na kandarasi ya miaka miwili.

Dirisha la uhamisho wa wachezaji barani Uropa linafungwa rasmi tarehe mbili Septemba.

Show More

Related Articles