MichezoMilele FmSwahili

Shujaa wapata alama 5 Las Vegas

Timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande ilifaulu kupata alama tano katika michezo iliotamatika jana kule Las Vegas Marekani.

Alama hizo tano zilipatikana katika ushindi wa 24 kwa 19 dhidi ya Argentina kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B,na ushindi pia wa alama 28 kwa 15 dhidi ya Japan katika robo fainali ya taji la Challenge.

Licha ya matokeo hayo ya Las Vegas,timu hiyo ya shujaa chini ya Mwalimu Paul Murunga inasalia katika nafasi ya 13 kwa alama 17.

Timu hiyo italenga kujiimarisha zaidi wikendi ijayo katika mkondo wa sita kule Vancouver Canada

Show More

Related Articles