HabariMilele FmSwahili

Serikali yatuma wataalamu kujiunga na wale wa Ethiopia kubaini kiini cha ajali ya ndege ya Boeing 737

Serikali imetuma kundi la wataalamu kujiunga na wale wa serikali ya Ethiopia katika uchunguzi kubaini kiini cha ajali ya ndege ya Boeing 737. Waziri wa uchukuzi James Macharia anasema kundi hilo litaongozwa na mkurugenzi wa uchunguzi wa ajali za ndege kapteni Martyne Lunani pamoja na mkurugenzi wa usalama wa safari za anga kapteni Tom Ogeche. Macharia anasema wachunguzi hao pia wanajumuisha wanapatholojia wa serikali watakaosaidia kutambua miili ya wakenya walioangamia kweney ajali hiyo. Hadi sasa anasema familia za wakenya 25 kati ya 32 walioangamia kwenye ajali hii wamejuzwa na kupewa ushauri.

Kauli yake inawadia wakati katibu wake Esther Koimmet akikutana na uongozi wa serikali ya Ethiopia. Mkutano huo unalenga kuangazia  zaiid kuhusu jinsi utambulisho wa miili ya walioangamia kutokana na ajali hiyo utafanywa.

Wakati huo huo balozi wa kenya nchini Ethiopia Catherine Mwangi, pia anasema wametenga kituo maalum katika uwanja wa ndege wa Ethiopia kupokea familia wa walioangamia kaitka ajali hiyo.

Hayo yanajiri wakati serikali ya Uchina ikipiga marufuku safari zote za ndege Boieng 737 max 8. Utawala wa Beijing umenukuu ajali kadhaa ambazo zimehusishwa na ndege hiyo muda mchache tu baada ya kupaa angani, hivyo kuagiza zifanyiwe uchunguzi wa kina.

Show More

Related Articles