HabariMilele FmSwahili

Mwanamume afariki baada ya kubugia pombe haramu Litein, kaunti ya Kericho

Mwanamume mmoja ameaga dunia baada ya kubugia pombe haramu kiungani mwa mji wa Litein, kaunti ndogo ya Bureti.

Akithibitisha kisa hiki, OCPD Felicia Tengeya, anasema mwili wa marehemu aliyekuwa akiishi peke yake haukuwa na majeraha yoyoy akisema uchunguzi zaidi unaendeshwa.

Naibu kaunti kamishna Kevit Jilo naye amesema vita dhidi ya pombe haramu vimeimarishwa eneo hilo huku akitoa wito wa ushirikiano miongoni mwa wenyeji na maafisa wa usalama kufanikisha vita hivyo

Show More

Related Articles