HabariMilele FmSwahili

Mtu mmoja afariki kwenye ajali ya barabarani eneo la Kenyanya kaunti ya Kisii

Mtu mmoja amefariki katika ajali ya barabarani eneo la Kenyenya bara bara ya Etago-Mogonga kaunti ya Kisii baada ya kugongwa na lori.

Kulingana na ripoti kutoka kwa kamanda wa polisi kaunti ya Kisii Martin Kibet, lori hilo ambalo dereva alitoroka lilikuwa linatoka Mogonga kuelekea Etago kwa mwendo wa kasi kabla ya kupoteza mwelekeo na kuligonga gari dogo ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya bara bara likiwa na dereva ndani.

Marehemu amefariki baada tu ya kufikishwa katika hosipitali ya Kenyenya kupewa matibabu.

Show More

Related Articles