HabariMilele FmSwahili

Mtu 1 afariki baada ya kuzuka mkurupuko wa ugonjwa wa Anthrax Kisumu

Mtu mmoja amedhibitishwa kufariki na wengine 4 kuwa hali mahututi kaunti ya Kisumu baada ya kuugua ugonjwa wa kimeta almaarufu Anthrax. Idara ya afya kaunti ya Kisumu imedhibitisha kuzuka mkurupuko wa ugonjwa eneo la eneo la Mowlem huko Nyamasaria. Mkurugenzi wa afya kaunti hiyo Dickens Onyango anasema takriban watu 40 wameonyesha dalili saw na za ugonjwa huo baada ya kumla ng’ombe aliyeugua kimeta katika karamu mmoja Julai 5.

Aidha onyango ameagiza zahanati zote kaunti hiyo zitakazowapokea wagonjwa wa kimeta kuwasilisha ripoti kwake kwa tahadari kuchukuliwa

Show More

Related Articles