MichezoMilele FmSwahili

Mshambulizi Ephraim Guikan agura klabu ya Gor Mahia

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya KPL Gor Mahia wamepata pigo baada ya mshambulizi raia wa Ivory Coast Ephraim Guikan kugura klabu hiyo.

Mwendo wa saa tano usiku wa jana mshambulizi huyo alikamilisha mazungumzo ya kuigura Kogalo, na sasa anaelekea katika katika ligi ya Zambia.

Guikan amepata nafasi kuwa finyu ndani ya kambi ya Kogalo, haswa baada ya mkufunzi mkuu Hassan Oktay kuchukua hatamu za kuifunza timu hiyo.

Guikan anafuata nyayo za meddie kagere aliyehamia simba ya Tanzania, kando na Geoffery Walusimbi aliyesajiliwa na klabu ya kaizer chiefs ya Afrika Kusini.

Show More

Related Articles