HabariMilele FmSwahili

Matiangi aagiza ukaguzi wa wawekezaji wa kigeni

Kenya inazidai kampuni za kamari jumla ya shilingi bilioni 26. Ni kutokana na hili ambapo sasa waziri wa usalama wa taifa dkt Fred Matiangi ameagiza ukaguzi wa wawekezaji wote wa kigeni walioko nchini. Matiangi anasema baadhi ya wawekezaji hao wamekwepa kulipa ushuru. Kadhalika anasema licha ya kujihusisha na biashara ambazo hawajaidhinishwa,imekuwa vigumu kuwaandama  kutokana na amri za mahakama.

Akiongea kwenye mkao wa kujadili sheria zinazotarajia kudhibiti biashara hiyo,Matiang ameahidi kufikia tarehe 30 mwezi ujao leseni zote zinazotolewa kwa kampuni za kamari zitakaguliwa upya kuhakikisha zile zinazolipa ushuru ndizo zinaidhinishwa kuhudumu pekee.

Show More

Related Articles