HabariMilele FmSwahili

Jowie anyimwa dhamana

Mahakama kuu kwa mara nyingine imetupilia mbali ombi la mshukiwa wa mauaji Joseph Irungu almaarufu Jowie kuachiliwa kwa dhamana. Jaji James wakiaga ameamua kuwa ombi la Jowi halina msingi. Aidha ameagiza ombi hilo kuwasilishwa kwa mashahidi wote kuruhusiwa kuwasilisha ushahidi wao kabla ya mahakama kuliangazia. Mshukiwa huyo anakabilowa na shtaka la mauaji ya Monica Kimani mwaka jana hapa jijini Nairobi, shtaka ambalo tayari amekana.

Show More

Related Articles