HabariMilele FmSwahili

Mahakama kutoa uamuzi wa kesi ya kupinga uchaguzi wa gavana Waiguru

Mahakama ya upeo hii leo inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusiana na kesi ya uchaguzi wa gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru uliopingwa na kinara wa chama cha Nark Kenya Martha Karua.

Karua anadai uchaguzi huo ulikumbwa na dosari hali iliyopelekea Waiguru kuibuka mshindi kwa kujizolea kura 153533.

Hata hivyo mahakama kuu na ile ya rufaa hapo awali zilitupilia mbali kesi hiyo kwa madai hakukuwa na ushahidi wa kutosha kutupilia mbali ushindi wa Waiguru.

 

Show More

Related Articles