HabariMilele FmSwahili

Magunia 446 ya sukari ghushi yanaswa eneo la Chokaa , Nairobi

Maafisa wa idara ya upelelezi wamefanikiwa kunasa magunia 446 ya sukari ghushi eneo la Chokaa hapa jijini Nairobi.

Maafisa hao pia wamefanikiwa kuwanasa watu watano waliokuwa wakipakia sukari hiyo inayoshukiwa kutoka eneo la Magharibi mwa Kenya kwenye magunia hayo yaliyoandikwa siyo ya kuuza.

Washukiwa Hassan Ibrahim, Geoffrey Mutua, Moses Murigi Irungu, Elkana Waro Omache na Nancy Wanja kitonga wanatarajiwa kufikishwa mahakamani huku uchunguzi zaidi ukiendeshwa dhidi ya sukari hiyo.

Show More

Related Articles