MichezoMilele FmSwahili

Kenya yatinga fainali ya Vikapu Bamako

Timu ya taifa ya mchezo wa mpira wa vikapu imefuzu kwa fainali ya mashindano ya Bara Afrika mjini Bamako Mali baada ya kuicharaza Morocoo alama 96 kwa 66 jana usiku kwenye nusu fainali ya kwanza.

Nyota wa Kenya Eric Mundoro alikuwa mahiri katika mchezo huo akifaulu kufunga vikapu 29.

Timu hiyo sasa itamenyana na DRC katika fainal kesho usiku na itakuwa mara ya pili timu hizo mbili kupepetana baada ya kutoa kijasho kwenye hatua ya makundi.

DRC imejikatia tiketi ya fainali kwa kuilabua Angola vikapu 84 kwa 78.

Mchezaji wa Morans Tylor Ongwae anaongoza chati ya wafungaji bora wa michezo hiyo kwa jumla  ya alama 109.Michael Koibe wa Chad ni wa pili kwa alama 93.

Matokeo ya awali ya timu hiyo

Kenya 65-82 DRC

Kenya 81-69 Nigeria

Kenya 85-83 Ivory Coast

Kenya 82-76 Tunisia

 

Show More

Related Articles