HabariMilele FmSwahili

Kamati ya uhasibu bungeni kuchunguza upya sakata ya ardhi ya Ruaraka

Kamati ya bunge kuhusu uhasibu itaendesha uchunguzi upya kuhusiana na utata unaozingira ardhi ya ekari 13.5 ya Ruaraka hapa Nairobi. Ni baada ya mkaguzi mkuu wa serikali Edward Ouko kutilia shaka jinsi tume ya ardhi iliidhinisha malipo ya shilingi bilioni 1.5 kati ya bilioni 3.3 kwa mfanyibiashara Francis Mburu aliyedai kumiliki ardhi hiyo ilio makao ya shule za Drive in na Ruaraka high mtawalia. Akiongea na Milelefm,mwenyekiti wa kamati hiyo Opiyo Wandayi anasema kamati yake itaendesha uchunguzi huru kubaini nini hasa kilijiri hadi kupelekea mburu kulipwa fedha hizo licha ya uchunguzi wa awali kuonyesha ardhi hiyo ilikua ya serikali. Ripoti ya mkaguzi wa serikali ilifichua kwamba hata Mburu angekua mmiliki wa ardhi hiyo, hakustahili kulipwa shilingi bilioni 3.3 na hiyo ilikua njama ya kupora mali ya umma.

Show More

Related Articles