HabariMilele FmSwahili

Huduma za matibabu katika hospitali ya Kenyatta zatatizika baada ya wafanyikazi kugoma

Viongozi wa wafanyikazi katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta  wanashiriki mkao na  mwenyekiti wa bodi ya  hospitali hiyo Nicholas Gumbo kutatua utata unaozingira marupurupu yao.

Awali wafanyikazi hao wameshiriki maandamano na kutatiza shughuli kwenye hospitali hiyo wakidai kukosa kupewa marupurupu yao ya miaka 6.

Wakioongozwa na katibu wao Albert Njeru  wanaulaumu usimamizi wa hospitali ya Kenyatta  wakisema umekuwa kikwazo katika utekelezaji wa agizo lililotolewa na  wizara ya afya kuwapa nyongeza.

Wanadai wamesusia kazi baada ya juhudi zao kupata suluhu kwa mvutano huo kukosa kuzaa matunda.

Wanasema mkuu wa hospitali hiyo amejifaidi na kukosa kutekeleza agizo la kupandisha  mishahara ya wafanyikazi wengine  baada ya hospitali ya Kenyatta kupandishwa hadhi.

Show More

Related Articles