HabariMilele FmSwahili

Maseneta walishtaki bunge la taifa kwa kupasisha miswada 20 bila kuwajumuisha

Kesi ya maseneta wanaotaka miswada 20 iliyojadiliwa na kupitishwa na bunge la taifa kubadilishwa imewasilishwa kwa jaji mkuu David Maraga kubuni jopo ili kutathmini lalama hizo. Jaji wa mahakama kuu Weldon Korir aliyepokea kesi hiyo baada ya maseneta kutembea kutoka majengo ya bunge hadi mahakamani humo, aidha ameiratibu kama ya dharura akitarajiwa kuitaja tena Julai 29. Wakizungumza baada ya kuwasilisha kesi hiyo, maseneta wakiongozwa na mawakili wao seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na seneta wa Siaya James Orengo, wanadai kuhujumiwa na wabunge licha ya kutambulika kama gurudumu kuu  la ugatuzi.

Maseneta waliotembea mwendo huo, wakiwa wameshikana mkono wameapa kushinikiza heshima kutoka kwa wenzao wabunge wamegusia zaidi mtafaruku kuhusu mgao wa serikali za kaunti

Show More

Related Articles