HabariPilipili FmPilipili FM News

Huduma Katika Soko Kuu Mjini Kilifi Za Dorora

Wafanyi biashara katika soko  kuu mjini Kilifi la Oloitiptip ,wamelalamikia kuzorota kwa biashara kutokana na huduma duni wanazopata kutoka kwa maafisa wa baraza la mji.

Wengi wao wameeleza kupitia changamoto nyingi katika soko hilo  ikiwemo kukithiri kwa mrundo wa taka ambao umechangia  baadhi ya maduka kufungwa.

Aidha wamelalamikia ukosefu wa usalama, mataa nyakati za usiku pamoja na ada za juu wanazotozwa kila mwezi.

Also read:   Wanafunzi Waungana Kilifi ili Kuendeleza Kaunti Hiyo Kimasomo

Wamemtaka gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi kuingilia kati ili kuhakikisha ada hizo zinapunguzwa na huduma kuimarishwa.

Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker