Prof Githu Muigai ajiuzulu kama Mwanasheria Mkuu 

Prof Githu Muigai ajiuzulu kama Mwanasheria Mkuu 

Mwanasheria mkuu Prof. Githu Muigai sasa amejiuzulu wadhifa wake.
Kulingana na ujumbe kwa vyombo vya habari kutoka kwa rais Uhuru Kenyatta, Muigai amejiuzulu  baada ya kuhudumu kwa miaka sita, na sasa nafasi hiyo  imependekezwa kuchukuliwa na jaji wa mahakama ya rufaa Paul Kihara Kariuki.
Hata hivyo kama anavyotuarifu Kiama Kariuki, hatua ya Kenyatta hii leo bila shaka ni ya kubadilisha kikosi chake kizima cha ushauri wa kisheria, ambacho kinasemekana kumfeli rais Kenyatta katika muhula wake wa kwanza.

Also read:   Mahakama ya Upeo yashindwa kusitisha uchaguzi wa Alhamisi

Related posts

MNL App
MNL App