TSC yawaorodhesha walimu wa kuhojiwa kwa ajira

TSC yawaorodhesha walimu wa kuhojiwa kwa ajira
Photo: Milele Digital

Tume ya kuwaajiri walimu TSC imeorodhesha  walimu 27,214 watakaohojiwa  kujaza nafasi 10,000 katika kundi la K,M,N. Nafasi hizo  zilitangazwa wazi mwezi Septemba mwaka jana. Walimu hao wanajumuisha walimu  wa shule za msingi  na manaibu wa wakuu ambao wamekuwa wakihudumu kama viwango vya G na H ambao wameongeza masomo na kupata cheti cha digrii. Wengine ni  walimu manaibu wa walimu wakuu na walimu wakuu katika  kundi la L ambao  watahojiwa na kupandishwa cheo  hadi kundi la M. Mwezi Agosti mwaka jana  tume hiyo ilipandisha vyeo  walimu 5,171 hadi kundi la H na J.

Also read:   Burundi yapiga marufuku makundi 10 ya kutetea haki za binadamu

Post source : Mediamax Digital

Related stories