Pigo kwa mpango wa serikali kuwaajiri madaktari kutoka Tanzania

Pigo kwa mpango wa serikali kuwaajiri madaktari kutoka Tanzania
Photo: Milele Digital

Chama cha madaktari nchini Tanzania kimepinga mpango wa Kenya kuwaajiri madaktari kutoka nchini humo. Katika taarifa chama hicho kinasema hakitakubali madaktari wa taifa hilo kuajiriwa hadi serikali ya Kenya itakapoanza utekelezaji wa makubaliano kati yake na madaktari wa humu nchini. Aidha kinasema hakikushirikishwa katika hatua yeyote na hivyo kukosa fursa yakufahamu lolote kuhusu mpango huo. Taarifa hii inakujia saa chache tu baada ya serikali kutetea uamuzi wake wa kuwatafuta madaktari kutoka Tanzania, Cuba na mataifa mengine.

Also read:   Almasi: Olivia Obell

Post source : Mediamax Digital

Related stories