HabariMilele FmSwahili

Bunge lapewa mwezi mmoja kutatua mgogoro kuhusu mgao wa fedha za kaunti

Mahakama ya juu imewapa wabunge na maseneta makataa ya mwezi mmoja kutatua mgogoro kuhusu ni pesa ngapi zitatengewa serikali za kaunti katika bajeti ya mwaka 2019/20.

Ni baada ya mabunge hayo kukosa kuwasilisha mkataba wa maelewano hii leo walivyotakiwa. Akitoa uamuzi huo,jaji mkuu David Maraga ameyataka mabunge hayo kusitisha misimamo yao mikali na kutatua mgogoro huo mara moja.

Maraga anasema, mahakama hiyo haitaingilia kati mgogoro huo kabla ya mbinu zilizopo kutumika inavyostahili.

Katika maombi yao,mawakili wa baraza la magavana,maseneta na tume ya ugavi wa mapato CRA wametaka kesi hiyo kuendelea na mahakama hiyo kutoa ushauri wake.

Hata hivyo,wabunge kupitia spika Justine Muturi wanataka vikao hivyo kusitishwa kwa siku 30 ili kuruhusu mazungumzo zaidi kufanyika.

Show More

Related Articles