BiasharaMilele FmSwahili

Benki kuu yadinda kuondoa faini iliyotoza benki 5 nchini kuhusiana na sakata ya NYS

Benki kuu imedinda kuondoa faini iliyotoza benki tano za humu nchini kwa tuhuma za kutumika kuhifadhi shilingi bilioni 3.5 zilizoporwa katika shirika la NYS. CBK ilidokeza benki za Standard Charterd, Equity, KCB, Coperative na Diamaond Trust Bank zilikiuka sheria dhidi ya ulanguzi wa fedha kwa kutumika kuhifadi pesa hizo. Kwa ujumla benki hizo zilitozwa faini ya shilingi milioni 392.5. Benki ya Standard Charterd shilingi milioni 77.5 kwa kuhifadhi shilingi bilioni 1.6 huku Equity ikitozwa milioni 89.6. benki ya KCB ilitozwa faini ya milioni 149.5 , Cooperative milioni 20 nna Diamond Trust Bank milioni 56.

Show More

Related Articles