HabariMilele FmSwahili

Ada ya kuegesha magari jijini Nairobi yapunguzwa hadi shilingi 200

Madereva jijini Nairobi wamepata afueni baada ya serikali ya kaunti kupunguza ada ya kuegesha magari. Gavana Mike Sonko ameagiza ada hiyo kupunguzwa kutoka shilingi 300 hadi 200 kwa siku. Agizo hilo litaanza kutekelezwa Jumatatu Juma lijalo. Madereva wamekuwa wakilipa shilingi 300 tokea mwaka wa 2013. Aidha pendekezo la kaunti kuongeza ada hiyo hadi shilingi 400 mwama jana lilitupiliwa mbali kufuatia mazungumzo baina ya serikali ya kaunti na wadau walioazimia kupunguzwa kwake.  Gavana Sonko tayari ameelezea imani kuwa kupunguza ada hakutaongeza msongamano jijini kutokana na mpango wa kuanzisha huduma ya mabasi ya kusafirisha abiria wengi

Show More

Related Articles