Maafisa wa trafiki kuendesha misako dhidi ya madereva walevi wikendi hii

Maafisa wa trafiki kuendesha misako dhidi ya madereva walevi wikendi hii
Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet

Maafisa wa trafiki wataendesha misako dhidi ya madereva walevi katika maeneo mbali mbali wikendi hii. Inspekta jenerali Joseph Boinnet amewaonya wanaonuia kukiuka sheria baada ya kufurushwa barabarani maafisa wa NTSA. Boinet anasema maafisa wake watazidi kushirikiana na wale wa NTSA ili kudumisha usalama barabarani. Kadhalika amekanusha kuwepo mtafaruku baina ya maafisa wake na NTSA hali iliochangia kuondolewa kwao barabarani.

Also read:   Wanaharakati Katika Kaunti Ya Taita Taveta Waridhishwa Na NTSA Kuondolewa Barabarani

Post source : Milele fm

Related posts

MNL App
MNL App