HabariMilele FmSwahili

Raila awaomba wafuasi kujisajili kama wapiga kura

Wafuasi wa upinzani wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kama wapiga kura. Kinara wa upinzani Raila Odinga amewataka pia kujitokeza na kushiriki upigaji kura. Akizungumza katika mkutano ulioandaliwa katika ukumbi wa bomas muda mfupi uliopita Raila ametaka wafuasi wao wawe macho wakati wa ukaguzi wa sajili ya wapiga kura na kukabili mianya yoyote ya wizi wa kura. Kinara mwenza wa CORD Kalonzo Musyoka naye amesema yuko tayari kujiondoa kutoka kinyang’anyiro cha urais na kumpa nafasi atakayechaguliwa japo ametaka wenzake kufuata mkondo huo.

Also read:   Seneta Linturi awasilisha kesi mahakamani kuzuia chuo cha Nairobi kufutilia mbali usajili wake
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker