HabariPilipili FmPilipili FM News

Wazazi katika Kaunti Ya Kwale Waombwa Kutilia Elimu Maanani

Licha  ya serikali  kuahidi kuwachukulia  hatua za kisheria wazazi ambao hawapeleki watoto wao shuleni , bado asilimia kubwa ya watoto walio na umri wa kwenda shule  katika wadi ya mwereni ,lungalunga kaunti ya kwale  wamesalia nyumbani.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Naseriani eneo hilo  Salim Rashid  Charo anasema wazazi bado hawajatilia  maanani elimu,  licha ya masomo ya shule za msingi na upili kuwa bila malipo .

Charo ametaka jamii ihamasishwe zaidi kuhusu elimu kuona kuwa watoto wanapata msingi bora  wa maisha  yao ya badae.

Show More

Related Articles