HabariPilipili FmPilipili FM News

Wauzaji Vitabu Mombasa Wagadhabishwa Na Kuahirishwa Kwa Mtaala Wa 2-6-6-3.

Wauzaji wa vitabu mjini  Mombasa wameelezea masikitiko yao kwa serikali kwa kuahirisha uzinduzi wa mtala wa 2-6-6-3.

Wauzaji hao wanasema walikuwa wamenunua vitabu vya daraja la kwanza ,la pili na la tatu wakishindwa watakakovipeleka.

Wauzaji hao wanasema wameachwa njia panda huku wakilalamikia hasara ya mali yao.

Wazazi waliojitokeza kwa maduka ya vitabu wameonekana kukanganyika kuhusu vitabu wanavyofaa kuwanunulia watoto wao.Wanailaumu serikali kwa kukosa kuwaandaa kisaikolojia huku wakielezea hasara ya kununua vitabu vingine vivpya.

Show More

Related Articles