MichezoPilipili FmPilipili FM News

Wanadada Wa Bandari Waanza Vyema Kusaka Ubingwa Wa Mpira Wa Vikapu Nchini

Kina dada wa mchezo wa mpira wa vikapu wa kilabu ya Bandari (KPA) wamefanikiwa kushinda mechi yao ya kwanza kati ya mechi tano za mchujo kubaini bingwa wa kitaifa kwa mchezo huo nchini.

Warembo hao wa KPA waliweza kuwabamiza vikapu 57 kwa 47 wahifadhi fedha wa benki ya Equity kwenye ukumbi wa KPA Makande mjini Mombasa.

Kwenye msururu huo wa mechi tano timu itakayoshinda mechi tatu kawaida hutangazwa bingwa moja kwa moja na kwa mwenendo huu timu ya KPA inapaswa kushinda mechi mbili ili kutawazwa mabingwa wa mchezo huo.

Mkufunzi mkuu wa wanadada hao John Ojwuku amewasifia kwa ukakamavu wao na kuhakikisha wanautumia uwanja wa nyumbani kuwalaza wapinzani wao.

Kwa uoande wake mkufunzi wa klabu ya Equity   bwana Maina hukusita kuwalaumu wachezaji wake kwa kuwa wabinafsi katika mechi hio jambo ambalo anasema limesababisha wao kupoteza mechi hio.

Leo timu hizo zitaingia tena dimbani kukabilina kwa mechi ya pili kwenye ukumbi wa KPA Makande kabla ya kusafiri kukabilia kwa mechi tatu zilizosalia jijini Nairobi ili kubaini bingwa wa kitaifa.

Tayari wanaume wa timu ya vikapu ya KPA ndio mabingwa wa kitaifa mwaka huu baada yakuwarindima Ulinzi wikendi iliyopita.

 

Show More

Related Articles