HabariPilipili FmPilipili FM News

Walimu Waliostaafu Bado Wanaidai Serikali Bilioni 42.3.

Jumla ya walimu elfu 52 waliostaafu sasa wanaitaka serikali kuwalipa shilingi bilioni 42.3 , pesa hiyo  ikiwa ni salio ya mishahara na marupurupu yao ya uzeeni.

Walimu hao waliostaafu chini ya kundi la mwaka wa 1997, wanadai serikali imekuwa ikikwepa kuwapa pesa zao licha ya mahakama kuagiza walipwe tangu mwaka wa 2008.

Aidha wanasema pesa hizo zimekuwa zikizaana kwa riba ya asilimia 14 kila mwaka, tangu agizo hilo kutolewa na jaji David Maraga mnamo mwezi wa Octoba mwaka wa 2008.

Inaarifiwa zaidi ya wanachama 2,000 wa kundi hilo wamefariki bila ya kupata pesa zao.

Show More

Related Articles