BiasharaPilipili FmPilipili FM News

Wakulima Wa Miwa Waitaka Serikali Kutoagiza Sukari Kutoka Nje.

Wakulima wa miwa sasa wanaitaka serikali izuie kabisa uagizaji wa sukari kutoka mataifa ya kigeni ili kuinusuru sekta hiyo humu nchini.

Wakulima hao aidha wanailamu serikali kwa kuchelewesha malipo yao.

Waziri wa kilimo Mwangi kiunjuri  hata hivyo anasema ameiandikia wizara ya fedha kuachilia shilingi bilioni 2.6 ili kuwalipa wakulima hao wa miwa.

Aidha anasema wamebuni jopokazi la kuchunguza utata unaozingira sekta ya sukari , akiongeza kuwa ni lazima wakulima hao wakubali kukaguliwa ili kubainisha wakulima halali kabla ya wao kulipwa.

Hayo yakijiri waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri angali anasubiri shilingi bilioni 2.1 za kuwalipa wakulima wa mahindi.

Show More

Related Articles