HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakulima Katika Eneo La Mnagoni Huko Ganze Waishi Na Hofu.

Hofu imetanda katika eneo la Mnagoni kaunti ndogo ya Ganze baada ya wafugaji wa kuhamahama kumvamia mwenyeji ambaye  ni mkulima wa mmea na kumjeruhi vibaya.

Jumaa Mwambogo amejeruhiwa kwa kuchinjwa kwa visu na wafugaji hao baada ya  kuwazuilia mifugo wao kulisha katika shamba lake.

Mwambogo hata hivyo amepata usaidizi kutoka kwa wananchi wengine baada ya yeye kuanguka chini na kupaza sauti za usaidizi.

Mkuu wa polisi katika eneo la Ganze Patrick Ngeiwya amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa uchunguzi umeanzishwa.

Kulingana na Ngeiwya maafisa wa serikali wanapanga kufanya mkutano baina ya wafugaji hao na wenyeji ili kusuluhisha mzozo huo.

Show More

Related Articles