HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakenya Kununua Unga Wa Sima Kwa Shilingi 90.

Wakenya watanunua unga wa mahindi wa kilo mbili kwa shilingi 90 kuanzia kesho.

Waziri wa kilimo Willy Bett anasema wananchi watapata unga wa kilo moja kwa shilingi 47.

Anasema hatua hiyo ni baada ya serikali kupunguza bei hadi shilingi 2,300 ambayo wasagaji unga wa mahindi watanunua mahindi ya kilo 90 kuanzia kesho.

Bett anasema hatua hiyo hailengi kupata faida yoyote ila kuhakikisha bidhaa hiyo inapatikana sehemu zote nchini na itaendelea hadi badaa ya kuvuna.

 

 

 

 

Show More

Related Articles