HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa Eneo La Kisauni Walalamikia Ukosefu Wa Usalama Katika Eneo Hilo.

Wakazi wa eneo la Kisauni hapa Mombasa wamelalamikia visa vya ukosefu wa usalama kwa madai kuwa wanaoshika doria wamekosa uaminifu kwao.

Hii ni baada ya visa kadha vya uhalifu kushuhudiwa ambapo watu watatu walipigwa na vifaa butu katika hoteli moja eneo hilo.

Aidha Peter mkaazi wa eneo hilo ameweza kuzungumza na meza yetu ya habari  na kukashifu vikali makundi ya kutetea haki kwa kukosa kukashifu uhalifu badala yake kukosoa polisi.

Ameongea haya kabla ya kikao cha baraza la usalama kitakachoongozwa na kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki kufanya eneo hilo leo.

Show More

Related Articles