HabariPilipili FmPilipili FM News

Wafanyibiashara Walalamikia Kubomolewa Vibanda Kongowea.

Shughuli za usafiri katika barabara za eneo la Lights hapa Mombasa zilitatizika kwa muda baada ya baadhi ya wafanyabiashara wa vibanda vya nguo katika soko la Kongowea kuandamana na kufunga barabara hizo kwa kuchoma magurudumu wakilalamikia hatua serikali ya kaunti ya Mombasa ya kuwavunjiwa vibanda vyao bila ilani yoyote

Wakizungumza na wanahabari hii leo wamesema hawakupewa ilani ya kuondoa bidhaa zao na wengi wao wana madeni ya kulipa karo za shule na mikopo ya biashara ambayo hawataweza kulipa kufuatia hasara ya kuharibiwa kwa mali zao.

Aidha wamesema wamefanya kazi  sehemu hiyo zaidi ya miaka kumi na hawajui ni kwanini serikali ya kaunti inawaondoa bila kuwatengea sehemu nyengine ya kufanya kazi.

Hata hivyo wengine wamesema swala la siasa limechangia vibanda vyao kuondolewa.

 

Show More

Related Articles