HabariPilipili FmPilipili FM News

Viongozi Wahimizwa Kushirikiana Kuukabili Ufisadi.

Himizo limetolewa kwa viongozi kushirikiana pamoja katika kulikabili janga la ufisadi ambalo limekuwa likifyonza mabilioni ya fedha za wananchi.

Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime anasema ufisadi utaweza kukabiliwa pale mikakati ya pamoja itawekwa na asasi zote husika, ikiwemo idara ya mahakama kuwajibikia majukumu yake kikamilifu.

Anasema endapo hilo litakosa kuangaziwa mabilioni ya fedha za wakenya zitaendelea kufujwa na wachache wasiojali maendeleo ya taifa.

Show More

Related Articles