HabariPilipili FmPilipili FM NewsSwahili

Viongozi Wa Pwani Waeleza Matumaini Ya Kushinda Urais 2022.

Azma ya viongozi wa pwani kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha Urais kwenye uchanguzi mkuu mwaka 2022 inaendelea kushika kasi huku magavana wa Mombasa Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi wakishauriwa kufanya mazungumzo ya atakayeipeperusha bendera hiyo ikizingatiwa kuwa wote wametangaza kukigombea kiti hicho. Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire anasema mashauriano ya wawili hao yatawawezesha viongozi kutoka pwani kuwa na nguvu zaidi ya kumpigia debe mmoja wao.

Kauli sawa imetolewa na  mbunge wa Rabai William Kamotti, ambaye amewarai viongozi waliokiasi chama cha ODM kurejea chamani humo ili kupiga jeki azma ya chama kutwaa uongozi wa taifa ujapo uchaguzi mkuu mwaka wa 2022.

Wito wa Kamoti umeungwa mkono na mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi.

Show More

Related Articles