MichezoPilipili FmPilipili FM News

Uingereza Yanyakua Kombe La Dunia Kwa Wachezaji Wasiozidi Umri Wa Miak 20.

VIJANA wa England wa chini ya Miaka 20 ndio Mabingwa wa Dunia baada ya kubeba Kombe la Dunia kwa Vijana wa chini ya Miaka 20, U-20, kwa kuibwaga Venezuela 1-0 kwenye Fainali iliyochezwa huko South Korea.

Bao la ushindi la England lilifungwa Dakika ya 35 na Mchezaji wa Everton Dominic Calvert-Lewin huku Kipa wa England, anaedakia Newcastle, Freddie Woodman, akiokoa Penati ya Kipindi cha Pili iliyopigwa na Adalberto Penaranda.

Penati hiyo ilitolewa zikibakia Dakika 17 kufuatia rafu ya Kyle Walker-Peters kwa Penaranda na Refa kuthibitisha kuwa ni Penati halali baada kutumia VAR, Msaada wa Video, ambao umekuwa ukitumika kwa Majaribio kwenye Mashindano haya.

Hii ni mara ya kwanza kwa England kutwaa Kombe kubwa tangu Timu ya Kwanza yao kubeba Kombe la Dunia Mwaka 1966 Mjini Wembley Jijini London.

VIKOSI:

Venezuela (4-4-2): Farinez; Hernandez, Ferraresi, Velasquez, Hernandez; Cordova, Lucena, Herrera, Penaranda; Pena, Chacon.

England (4-3-3): Woodman, Kenny, Clarke-Salter, Tomoki, Walker-Peters; Cook, Onomah, Dowell; Calvert-Lewin, Solanke, Lookman.

Show More

Related Articles