HabariPilipili FmPilipili FM News

Tutaendelea Kuwakabili Wahalifu Asema Ipara.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara amethibitisha kuwa Ali Athman aliyepigwa risasi kwenye upande mmoja wa shingo ,na bega jana jioni eneo la Barsheba Kisauni, ni mwanachama wa magenge ya vijana ambayo yamekuwa yakiwahangaisha wakazi wa eneo hilo.

Ipara amesema Athman mwenye umri wa miaka 28 ambaye anaendelea kutibiwa katika hospitali moja mjini Mombasa  chini ya ulinzi mkali wa polisi, alipigwa risasi baada ya jaribio lake na wenzake 20 waliofanikiwa kutoroka la kuwavamia polisi kwa panga na visu kutibuka.

Ipara amesema polisi wamefanikiwa kupata panga 4 na visu 6 eneo la tukio hilo, akiongeza kuwa Athman atasadia Polisi kuwakamata wanachama wengine wa magenge hayo ambao wamekuwa wakitatiza usalama eneo bunge la Kisauni.

Amedokeza kuwa awali Polisi waliokuwa wakishika doria eneo hilo walilazimika kufyatua risasi hewani ili kuwakabili wanachama hao ambao miongoni mwao walitoroka huku wengine akiwamo Athaman kuamua kuwavamia Polisi.

Anasema idara yake haitolegeza kamba katika kuwakabili wahalifu ambao wamekuwa kero kwa wakazi wa Kisauni kwa hapa mombasa.

Hayo yanajiri siku 7 baada ya watu watatu kufariki dunia kufuatia uvamizi uliotekelezwa na  wanachama wa magenge hayo eneo la Junda Kajiweni eneo bunge hilo.

Show More

Related Articles