BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Tamasha La Tatu La BYOB Summit Langoa Nanga Hapa Mjini Mombasa.

Zaidi ya vijana 8,000 kutoka ukanda wa pwani wanatarajiwa kupata uhamasisho wa taaluma mbali mbali hapa mjini Mombasa.

Hii ni baada ya kampuni ya safaricom kuandaa tamasha kubwa linalofahamika BYOB summit katika uwanja wa Mombasa sports club.

Wakati wa tamasha hilo vijana mbali mbali watahamasishwa na wataalamu mbali mbali wakiwemo wa maswala ya kilimo, uigizaji,uimbaji na wengineo.

Pia wasanii wa kutoka nchini akiwemo Timmy TDat, khaligraph Jones,  ohms law montana huku msanii maarufu kutoka nchini Tanzania Harmonize akitarajiwa kufunga tamasha hilo ambalo lineanza saa mbili na linatamatika saa kumi na moja jioni.

Show More

Related Articles